Psalms 79

Maombi Kwa Ajili Ya Wokovu Wa Taifa

(Zaburi Ya Asafu)


1 aEe Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako,
wamelinajisi Hekalu lako takatifu,
wameifanya Yerusalemu kuwa magofu.

2 bWametoa maiti za watumishi
kuwa chakula cha ndege wa angani
na nyama ya watakatifu wako
kwa wanyama wa nchi.

3 cWamemwaga damu kama maji
kuzunguka Yerusalemu yote,
wala hakuna yeyote wa kuwazika.

4 dTumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu,
cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka.


5 eHata lini, Ee Bwana? Je, wewe utakasirika milele?
Wivu wako utawaka kama moto hadi lini?

6 fMwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali,
juu ya falme za hao wasioliitia jina lako,

7 gkwa maana wamemrarua Yakobo
na kuharibu nchi ya makao yake.

8 hUsituhesabie dhambi za baba zetu,
huruma yako na itujie hima,
kwa maana tu wahitaji mno.


9 iEe Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,
kwa ajili ya utukufu wa jina lako;
tuokoe na kutusamehe dhambi zetu
kwa ajili ya jina lako.

10 jKwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wenu?”
Mbele ya macho yetu,
dhihirisha kati ya mataifa
kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa
ya watumishi wako.

11 kKilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako;
kwa nguvu za mkono wako
hifadhi wale waliohukumiwa kufa.


12 lWalipize jirani zetu mara saba vifuani mwao
aibu walizovurumisha juu yako, Ee Bwana.

13 mNdipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako,
tutakusifu milele;
toka kizazi hadi kizazi
tutasimulia sifa zako.
Copyright information for SwhKC